| Utume wetu Watawa wa Shirika la Mtakatifu Benedikto, wanaishi kulingana na Kanuni ya Mtakatifu Benedikto ambayo inadai maisha ya Sala na Kazi. Wakiungana na watu wengine wenye matashi mema, wanatafakari Neno la Mungu na kuadhimisha ukweli huo pamoja katika Sala na Adhimisho la Misa Takatifu. Zaidi ya hayo, wanajibidish katika kuhubiri, kufundisha na kufanya shughuli zingine mbalimbali kulingana na utume wao. Lengo lao ni kuibadili dunia ili iwe mahali bora pa kufaa kwa kila mtu na pia kuwafaidia watu wote kutokana na huduma zao. Utume wao unawasukuma kuwahudumia watu wote na kuwafanya wamoja katika Mungu. |
|