|
Nyumbani |
Mahali Maalum
|
Historia |
Schule |
Afya | Yatima |
Out Stations |
Musik
CD |
Mgusano & Msaada
Sr. Constatia
Sr. Valeria
Historia Kifupi ya Peramiho, Sehemu ya I Historia II -> Historia III -> Mwanzo Mgumu Tarehe 1 Julai, 1901, Masista 4 wa Shirika la Wamisionari Wabenediktini wa Tutzing Sr. M. Constantia Mayr OSB, Sr.M. Valeria Kuhlman OSB, Sr. M. Mechtildis Dickhoff OSB na Sr. M. Magdalena Hessing OSB waliwasili Peramiho. Hapo nyumba ya masista wa Mtakatifu Sholastika ilianzishwa Peramiho. Wakati wa vita vya Maji Maji, 1905, vituo vya wamisionari vya kusini mwa Tanganyika viliathiriwa. Wapiganaji wa vita vya Maji Maji waliiharibu misioni ya Peramiho mwezi Septemba na masista iliwapasa kutoroka. Tarehe 14 Agosti, wakiwa njiani kutoka Kilwa kuelekea Peramiho, Askofu Cassian Spiss, mabruda 2 na masisista M. Felicitas Hiltner na M. Cordula Ebert, waliuawa katika eneo la Liwale. 1909 ¬- Baada ya hali kuwa tulivu Masista walirudi Peramiho. Hapo walitoa huduma ya kutibu wagonjwa katika hospitali na walianzisha shule ya wasichana iliyofikia idadi ya wanafunzi 110. 1911 - Serikali iliwakabidhi masista eneo la Morogoro ambako walifungua kituo cha kutibu na kuwatunza wakoma. Huduma ilipoanza zahanati ilikuwa na wagonjwa takriban 200. 1912 - Viongozi wa Shirika kutoka Nyumba Kuu Ujerumani walizuru kituo cha Peramiho. Hapo walijionea yaliyotendeka na waliyarekodi hususa juu ya watu wengi waliobatizwa katika misioni husika, imani kubwa ya watu kwa wamisionari, shughuli za masista za kutunza wagonjwa, kufundisha watoto shuleni, kuwaendeleza zaidi kimasomo na na kadhalika. |

