Nyumbani | Mahali Maalum | Historia | Schule | Afya | Yatima | Out Stations | Musik CD | Mgusano & Msaada
Historia Kifupi ya Peramiho
Sehemu ya III
Mabadiliko na Nyakati wa Siku Hizi
1971-1976 Uongozi ulikuwa mikononi mwa Sr. M Elizabeth Sarinas OSB toka Ufilipino. Kwa mara ya kwanza masista kutoka Ufilipino walikuja kusaidia Priorati ya Peramiho.
Kuanzia mwaka 1962 idadi ya masista imepungua hatua kwa hatua. Mwaka 1990 jumuia ilikuwa na masista 44. Kwa hiyo, masista walioishi katika vituo vya maparokiani katika majimbo ya Songea, Mbinga na Njombe walirudishwa katika makao ya priorati Peramiho, iliyokuwa awali ya majimbo 3.
Utamadunisho wa Shirika
Mwaka 1982 Mwafrika wa kwanza Mtanzania, leo Sr. M. Getrud Luoga wa Parokia Luwana Njombe, alijiunga na shirika la Masista Wamisionari Wabenediktini wa Tutzing Peramiho jambo ambalo lilileta sura mpya katika jumuia.
Malezi ya watawa watarajiwa ya wakati ule kule Nairobi, yalijumuisha wasichana kutoka nchi za kiafrika. Wakati ule wasichana waliokuwepo walitoka Kenya, Uganda, Nigeria, Angola na Tanzania.
Malezi ya hapa Tanzania Peramiho yalitoa tunda la kwanza tarehe 10 Februari 1996 pale Sr. M. Gloria Haule wa Jimbo Kuu la Songea na Sr. M. Odilia Kipanga wa Jimbo la Morogoro walipoweka Nadhiri za Kwanza katika Kanisa la Abasia.
Sasa malezi kwa ajili ya Priorati za Peramiho na Ndanda hufanyika hapa Peramiho.
| Wamama Wakubwa katika Wakati Huu | |
| 1963-1971 | Sr. Verediana Wolfsteiner, OSB |
| 1971-1976 | Sr. Elizabeth Sarinas, OSB |
| 1976-1987 | Sr. Isentrud Lehner, OSB |
| 1987-1995 | Sr. Maria Goretti Gast, OSB |
| 1995-2007 | Sr. Pia Portmann, OSB |
| 2007-Present | Sr. Rosann Ocken, OSB |
