MBS logo 12 kb   

Missionary Benedictine Sisters

Peramiho, TANZANIA, East Africa

Home | Location | History | Education | Health Care | Orphanages | Out Stations  | Music  | Contact

Nyumbani | Mahali Maalum | Historia | Schule | Afya | Yatima | Out Stations | Musik CD | Mgusano & Msaada

             Mt. Joseph Hospitali Peramiho

                                  Historia Kifupi I   

1901  Masista 4 Wamisionari Wabenediktini miongoni mwao mmoja akiwa nesi na wengine wasaidizi wa Uuguzi waliwasili Peramiho. Kundi hili la masista lilitoa huduma ya kuwatunza   wagonjwa wa vijijini. Aidha waliwatunza wakoma wa kituo kilichokuwa karibu na eneo la Lundusi Peramiho.

1909  Baada ya kuondoka Peramiho kwa sababu ya Vita vya Maji Maji, Masista walirudi Peramiho na wakaanza upya kufanya kazi zao. Nyakati zile wagonjwa walitibiwa Peramiho katika jengo la zahanati lililoezekwa nyasi. Wagonjwa wengine walitembelewa na kuhudumiwa kwenye makazi yao vijijini.

1911  Serikali ilijenga nyumba katika eneo la Morogoro kwa ajili ya kuishi wagonjwa wa ukoma na ikawakabidhi masista wahudumu jengo hilo.

1923  Kufukuzwa Wamisionari Wajerumani nje ya Tanganyika mwaka 1916 kulihitimisha kipindi cha kazi ya kimisionari kilichotangulia na kufungua kipya. Ili kuboresha huduma za afya, zilijengwa wodi za udongo kwa ajili ya kulala   wagonjwa. Kulitolewa mafunzo ya uuguzi kwa masista na wanakijiji kwa ajili ya huduma ya kituo cha afya. Dispensari zingine zilianzishwa katika maeneo ya Ungoni na Umatengo. Waganga wa hospitali ya wilaya ya Songea waliisaidia dispensari ya Peramiho kwa kutibu wagonjwa na kutoa ushauri.

1949  Hospitali Peramiho ilimpata Daktari Sr. M. Tetwigis Sailer OSB na hapo ikatunukiwa hadhi ya kuwa Hospitali.   Madaktari masista wengine waliongezwa; Sr. Maria Salus Linde OSB, Sr. Wernfried Walter OSB, Sr. Birgitta Schnell, OSB.

Mwaka 1952 Daktari Sr. Tetwigis, alianzisha Chuo cha Uuguzi hapo hapo Peramiho kwa ajili ya Mafunzo ya Uuguzi na Ukunga kwa muda wa miaka 4.