Hospitali ya Mtakatifu Yosefu Peramiho
1901 |
Masista 4 Wamisionari Wabenediktini miongoni mwao mmoja akiwa nesi na wengine wasaidizi wa Uuguzi waliwasili Peramiho. Kundi hili la masista lilitoa huduma ya kuwatunza wagonjwa wa vijijini. Aidha waliwatunza wakoma wa kituo kilichokuwa karibu na eneo la Lundusi Peramiho. |
|
1909 |
Baada ya kuondoka Peramiho kwa sababu ya Vita vya Maji Maji, Masista walirudi Peramiho na wakaanza upya kufanya kazi zao. Nyakati zile wagonjwa walitibiwa Peramiho katika jengo la zahanati lililoezekwa nyasi. Wagonjwa wengine walitembelewa na kuhudumiwa kwenye makazi yao vijijini. |
|
1911 |
Serikali ilijenga nyumba katika eneo la Morogoro kwa ajili ya kuishi wagonjwa wa ukoma na ikawakabidhi masista wahudumu jengo hilo. |
|
1923 |
Kufukuzwa Wamisionari Wajerumani nje ya Tanganyika mwaka 1916 kulihitimisha kipindi cha kazi ya kimisionari kilichotangulia na kufungua kipya. Ili kuboresha huduma za afya, zilijengwa wodi za udongo kwa ajili ya kulala wagonjwa. Kulitolewa mafunzo ya uuguzi kwa masista na wanakijiji kwa ajili ya huduma ya kituo cha afya. Dispensari zingine zilianzishwa katika maeneo ya Ungoni na Umatengo. Waganga wa hospitali ya wilaya ya Songea waliisaidia dispensari ya Peramiho kwa kutibu wagonjwa na kutoa ushauri. |
|
1949 |
Hospitali
Peramiho ilimpata Daktari Sr. M. Tetwigis Sailer OSB na hapo ikatunukiwa
hadhi ya kuwa Hospitali. Madaktari masista wengine waliongezwa;
Sr. Maria Salus Linde OSB, Sr. Wernfried Walter OSB, Sr. Birgitta Schnell
OSB. |
|
1980
- 2000 |
Ni kipindi cha mabadiliko makuu anuai: ujenzi wa majengo mapya, ukarabati wa majengo, ongezeko la idadi ya wagonjwa na madaktari bingwa, na uboreshaji wa tiba. Katika kipindi hicho hospitali ilikuwa na vitanda 420 na iliongozwa na daktari Br. Ansgar Stuefe OSB. Hospitali ilijiendeshea yenyewe Chuo cha Wauguzi na Ukunga ambacho kiliweza kupokea wanafunzi kuanzia 100 hadi 120. Awali wahitimu baada ya kozi ya miaka 4 walijipatia shahada. Toka mwaka 2004 wanachuo wakihitimu kozi yao walijipatia cheti cha Diploma au Stashahada. Tena kulitolewa mafunzo ya Wasaidizi wa Maabara kwa muda wa miaka 2. Wahitimu hutunukiwa Shahada la Wahudumu Wasaidizi wa Maabara. |
|
Wakoma Masista wetu walianza kukiendesha kituo na kuwahudumia wakoma tangu mwaka 1911 hadi sasa. Ufanisi wa huduma kwa kutoa dawa nzuri umefanikisha kutatua na kuponya shida mpya zilizojitokeza na idadi ya wagonjwa inapungua siku hadi siku isipokuwa shida za ulemavu wa shida za muda mrefu. Mintarafu Ukimwi, kumejitokeza changamoto la watoto yatima. Kwa hiyo sista mhudumu wa kituo amelazimika kufungua kituo cha Watoto Yatima ambao sasa wamefikia idadi takriban 120. Watoto hutunzwa kuanzia umri wa mtoto mchanga hadi wanapofikia umri wa kupata ajira. Kumlea kila mtoto kadiri ya mahitaji yake ni changamoto zito linaloshinikiza shirika letu hususan suala la gharama.
|
||
2003 |
Daktari Asngar Stuefe OSB aliondoka Peramiho na akahamia Ujerumani ambako alikabidhiwa wajibu mwingine katika shirika lake la Wamisionari Wabenediktini. Madaraka ya uongozi aliyakabidhi kwa Daktari Lemuel Rugumyamheto kama Naibu Mkurugenzi Mganga Mkuu na Daktari Venance Mushi kama Mganga Mkuu. |
|