Mahali tulipo na uwezekano wa kupatikana

 

Misioni ya Peramiho inapatikana katika Mkoa wa Ruvuma, kusini mashariki ya Tanzania katika wilaya ya Songea, kilometa 25 magharibi ya mji wa Songea. Barabara toka Peramiho/Songea hadi Dar-es-Salaam ni ya urefu wa kilometa 1100 ni ya lami na ina hali nzuri. Huduma ya usafiri toka Songea hadi Peramiho ni ya uhakika zikitolewa na mabasi ya abiria na teksi za watu binafsi.

Mkoa wa Ruvuma una ukubwa wa eneo la kilometa za mraba 38,600. Idadi ya wakazi wake ni takribani   1,000,000.

Makabila yaliyopo: Wangoni, Wamatengo, Wandendeule, Wanindi, Wanyasa na Wayao.

Dini zilizomo: Wakatoliki, Waislamu, Waprotestanti, na Waamini wa dini za Jadi. Makundi hayo yanahusiana baina yao kwa amani bila migogoro.

Mazao ya biashara: Kahawa, Mahindi, Tumbako, Maharagwe, Korosho Mpunga na Ngano.

Mazao ya chakula ni: Mahindi, Mihogo, Maharagwe, Ngano, Mpunga, Ulezi na Mtama.