Misioni:
Awali katika shughuli za misioni, masista waliwafundisha waseminari na wanawake waliotengwa kwa sababu za kimila zilizopinga kumuelimisha mwanamke kusudi aolewe na kuzaa watoto tu. Mikakati na utekelezaji wa shughuli za kimisionari vya masista miaka zaidi ya 100 iliyopita vinaendelezwa bado lakini kwa mbinu tofauti na zile za awali ambazo hutokana na mahitaji na mazingira ya Kanisa la mahali. Huduma zetu ni zifuatazo: Uwemba Njombe tunafundisha Katekesi, tunashiriki shughuli za Jumuia Ndogo Ndogo, za Shirika la Kipapa la Mtoto Yesu na Vijana; huduma ya wagonjwa mahospitalini na katika zahanati; usitawi wa Jamii, kutunza watoto yatima, na kuendeleza vyuo vya Maarifa ya Nyumbani hususan huko Uwemba Njombe. Sasa Priorati yetu ina nyumba ndogo huko Uwemba na Uliwa Njombe. Baada ya muda mfupi tutafungua nyumba nyingine Mji Mwema Songea katika Jimbo Kuu la Songea |
![]() Peramiho Secondary School |
|
![]() Uwemba Domestic School |