Historia ya Priorati ya Peramiho

   
1901
Tarehe 1 Julai Masista 4 wa Shirika la Wamisionari Wabenediktini wa Tutzing Sr. M. Constantia Mayr OSB, Sr.M. Valeria Kuhlman OSB, Sr. M. Mechtildis Dickhoff OSB na Sr. M. Magdalena Hessing OSB waliwasili Peramiho. Hapo nyumba ya masista wa Mtakatifu Sholastika ilianzishwa Peramiho.

Sr. Constatia, Sr. Valeria
1905

Wakati wa vita vya Maji Maji vituo vya wamisionari vya kusini mwa Tanganyika viliathiriwa.   Wapiganaji wa vita vya Maji Maji waliiharibu misioni ya Nyangao tarehe 29 Agosti na Peramiho mwezi Septemba na masista iliwapasa kutoroka. Tarehe 14 Agosti, wakiwa njiani kutoka Kilwa kuelekea Peramiho, Askofu Cassian Spiss, mabruda 2 na masisista M. Felicitas Hiltner na M. Cordula Ebert, waliuawa katika eneo la Liwale.

 

 


Sr. Mechitildis, Sr. Magdalena
1909

Baada ya hali kuwa tulivu Masista walirudi Peramiho. Hapo walitoa huduma ya kutibu wagonjwa katika hospitali   na walianzisha shule ya wasichana iliyofikia idadi ya wanafunzi 110.

1911

Serikali iliwakabidhi masista eneo la Morogoro ambako walifungua kituo cha kutibu na kuwatunza wakoma. Huduma ilipoanza zahanati ilikuwa na wagonjwa takriban 200.

 
1912
Viongozi wa Shirika kutoka Nyumba Kuu Ujerumani walizuru kituo cha Peramiho. Hapo walijionea yaliyotendeka na waliyarekodi hususan juu ya watu wengi waliobatizwa katika misioni husika, imani kubwa ya watu kwa wamisionari, shughuli za masista za kutunza wagonjwa, kufundisha watoto shuleni, kuwaendeleza zaidi kimasomo na na kadhalika.  
1916

Vita Vikuu vya I vya Dunia vilisababisha masista waondoke tena nchini na kwenda Afrika ya Kusini. Mwaka 1920 masista walianzisha huko nyumba yao mpya.

 
1923

Masista Wabenediktini wasio wa taifa la Kijerumani waliwasili Peramiho kuendeleza kazi ya kimisionari iliyoachwa wazi na masista walioondoka. Wakati huo huo wasichana wenyeji waliopenda kuishi maisha ya kimonaki walianza kupata malezi yaliyotolewa na masista wamisionari. Mwaka 1938, baada ya kukua, Shirika la Watawa Wabenediktini wenyeji wa Mtakatifu Agnes lilianzisha makao yake mapya huko Chipole.

 
1926

Masista Wajerumani waliruhusiwa tena kuingia nchini kuendeleza huduma yao ya kimisionari. Shirika lilikua kwa kasi chini ya uongozi wa Abate Gallus aliyekuwa Kiongozi wa wakati ule. Masista walianzisha Chuo cha Ualimu, Chuo cha Ufundi fani ya Ushonaji na waliviendesha vyuo hivyo hadi pale mapadre na mabruda walipochukua nafasi ya kuviongoza na kuviendesha. Masista waliwafundisha waseminari wa kwanza somo la Kiingereza. Wakati wa kipindi cha uongozi wa Mama Priori M. Ermenilde Morrisey aliyesimikwa tarehe 26 Juni 1926, sister mmoja alikuwa mwalimu Mkuu wa shule ya msingi na mwingine aliongoza shule ya wasichana. Wakati Sr. M. Ermenilde akiwa   madarakani na Priorati ikiwa na masista takriban 60, zilifunguliwa nyumba 13 katika Parokia mbali mbali.       

 
   
1934 to 1939
Sr M. Agata Ross OSB aliongoza jumuia ya Mtakatifu Sholastika Peramiho.
1939 - 1947
Uongozi ulikuwa mikononi mwa Sr. M. Kunigunde Weber OSB akiwa kiongozi wa tatu.  
1947 - 1956
Sister M. Teodosia Biselli OSB alishika usukani.  
1956 - 1963
Sr. M. Paula Knoepfle OSB alichaguliwa kuwa kiongozi wa jumuia.
1963 - 1971
Jumuia ilikuwa chini ya Sr. M. Verediana Wolfsteiner OSB

left: Sr. Verediana, Sr. Elizabeth,
M. Gertrud
1971 -1976

Uongozi ulikuwa mikononi mwa Sr. M Elizabeth Sarinas OSB toka Ufilipino. Kwa mara ya kwanza masista kutoka Ufilipino walikuja kusaidia Priorati ya Peramiho.

1976 -1987

Kiongozi wa Jumuia ya Peramiho alikuwa Sr. M. Isentrud Lehner. Inakumbukwa kuwa wakati huu wasichana Waafrika walianza kualikwa kujiunga na shirika la Wamisionari Wabenediktini wa Tutzing ili kuendeleza kazi ya Umisionari kama Baba Benedikto anavyosisitiza ( Ora et labora yaani Sala na kazi ) na kukabili upungufu wa miito ya masista wamisionari toka Ulaya.
Wasichana waliojiunga Peramiho walitakiwa kwenda Nairobi kupata malezi yao kuanzia mwaka 1982 hadi 1995. Mwaka 1996 malezi yalifanyika hapa Tanzania.


Sr. Isentrud, Sr. Heimrada, Sr. M.Goretti, Sr. Elisabeth, Sr. Verediana
1987 - 1995
Priori wa Jumuia alikuwa Sr. M Goretti Gast OSB.
1995 -
Sr. M. Pia Portmann ni Priori wa jumuia yetu ya Peramiho


M. Irene OSB, Sr. Pia OSB

Kuanzia mwaka 1962 idadi ya masista imepungua hatua kwa hatua. Mwaka 1990 jumuia ilikuwa na masista 44. Kwa hiyo, masista walioishi katika vituo vya maparokiani katika majimbo ya Songea, Mbinga na Njombe walirudishwa katika makao ya priorati Peramiho.
Awali majimbo 3 ya   Songea, Njombe na Mbinga yalikuwa Jimbo la Abasia ya Peramiho. Leo ni majimbo matatu yaani Jimbo Kuu la Songea, Jimbo la Njombe na Jimbo la Njombe.

 

Utamadunisho wa shirika

Mwaka 1982 Mwafrika wa kwanza Mtanzania, leo Sr. M. Getrud Luoga wa Parokia Luwana Njombe, alijiunga na shirika la Masista Wamisionari Wabenediktini wa Tutzing Peramiho jambo ambalo lilileta sura mpya katika jumuia.

Malezi ya watawa watarajiwa ya wakati ule kule Nairobi, yalijumuisha wasichana kutoka nchi za kiafrika. Wakati ule wasichana waliokuwepo walitoka Kenya, Uganda, Nigeria, Angola na Tanzania.

Malezi ya hapa Tanzania Peramiho yalitoa tunda la kwanza tarehe 10 Februari 1996 pale Sr. M. Gloria Haule wa Jimbo Kuu la Songea na Sr. M. Odilia Kipanga wa Jimbo la Morogoro walipoweka Nadhiri za Kwanza katika Kanisa la Abasia.

Sasa malezi kwa ajili ya Priorati za Peramiho na Ndanda hufanyika hapa Peramiho.

 


Sr. Gertrud Luoga OSB


Sr. Gloria Haule OSB, Sr. Odilia Kipanga OSB