Utume wetu

Watawa Wabenediktini sisi bado tunafuata kanuni ya Mtakatifu Benedikto wa Nursia (karne ya 6). Muhtasari ya kanuni hii ni "Ora et labora et lege", maana yake "Sala na Kazi na Masomo". Kila siku inapata umbile yake kutokana na vipindi vya sala asubuhi, adhuhuri, jioni na mwanzo wa usiku. Kutokana na utulivu na uzoefu wa sala na kutokana na kusikiliza habari njema ya Injili tunapata nguvu ya kufanya kazi zetu.

Abasia yetu inategemea shirika la Wabenediktini Wamisionari wa St.Ottilien. Maana yake ni mwitu wa pekee kwa kuyasaidia makanisa yaliyoanzishwa karibuni na pia kwa kushirikiana miongoni mwa wakristu wote duniani. Tukifanya kazi mbalimbali vivandani, shuleni na za uchungaji, tunajaribu kutimiza miito hio. Aidha tunaelewa kazi yetu ni tendo la kimaendeleo ya kiuchumi katika nchi kwa ajili ya watu na maisha yao.


Mt.Benedikto wa Nursia (Picha ipo katika Sekondari ya Wasichana Peramiho)
St.Benedict of Nursia (Painting in Peramiho Girls' Secondary School)