Mauaji na Maangamizi
P. Cassian aliteuliwa kuwa askofu wa kwanza wa eneo la Wabenediktini mwaka 1902. Mwezi wa nane mwaka 1905 alisafiri kutoka Kilwa kwenda Peramiho. Alitarajia kumkuta Abate Norbert Weber wa St.Ottilien aliyekagua Peramiho kadiri ya sheria ya kanisa. Kabla hajaondoka Kilwa alitahadharishwa, lakini baadaye habari nyingine zilimpa moyo kusafiri. Porini karibu Liwale, mahali panapoitwa Mikukuyumbu, mwanzilishi wa Peramiho, pamoja na mabruda wawili, masista wawili na kijana mwanglikana walifia dini tarehe 14, mwezi wa nane, mwaka 1905. Waafrika wengine wa msafara walifaulu kutoroka, na wengine walishakimbia siku kabla yake. Walitaarifa kifo cha wamisionari Peramiho tarehe 26, mwezi huohuo.
Tarehe 03/09/1905 Nkosi Mputa Gama aliamuru kupiga ngoma za vita, wamisionari wakaamua kwenda misioni ya jirani, yaani Kigonsera. Paroko lakini, jina lake P. Franziskus Leuthner, alikataa kutengwa na wanaparokia. Tarehe 9 Wangoni waliangamiza Peramiho, P.Franziskus akauawa. Hivyo Mputa alilipiza shauri ya miaka miwili iliopita. Mwaka 1903 P.Franzikus alimlazimisha kuangamiza kibanda cha mahoga mbele wa watu wake.














Kuendelea
