Hawa ni mateka ambao ni wakubwa wa Wangoni kwa muda mfupi kabla ya kunyongwa huko Songea 27/02/1906. P.Johannes alipiga picha hii. Wao walikuwa 48 na wengi wao waliomba wabatizwe kabla ya kunyongwa miongoni mwao alikuwa Nkosi Mputa Gama ambaye alibatizwa (aliyekaa upande wa kulia wa mbele, aliyevaa kofia kichwani). P.Johannes alikuwa mtetezi wa moyo kwa wenyeji alipinga ukatili wa wakoloni, hadi mkuu wa serikali alidai kumhamisha. Picha hii pia inaitwa Mashujaa wa Wangoni.
Soma zaidi...