Viwanda vya abasia
Wakati walipofika wamisionari wa kwanza hapa Peramiho mnamo mwaka 1898, kila kitu kilitengenezwa na wamisionari wenyewe au kiliingizwa nchini kutoka Ulaya. Mfumo wa wafanyabiashara na mafundi ulikosekana. Hivyo mabruda walianzisha viwanda vikubwa vilivyohudumia mahitaji ya misioni na pia maendeleo ya nchi na elimu ya wazalendo. Hivyo viwanda bado vipo na vinatoa huduma kwa malengo hayohayo.
Kwa mfano: Useremala huko Uwemba
Nyumba ya Uwemba ina kitengo cha useremala. Msimamizi wa useremala huu ni Br.Kizito Nsafiri O.S.B., aliyefundishwa hapa Peramiho na marehemu Br.Albert na Br.Ignaz.
Kuna wafanyakazi watano. Kazi ikiwa nyingi, wafanyakazi wengine wanaajiriwa kwa muda. Wanatengeneza vitu mbalimbali: Milango, viti, meza, shelfi na kabati. Mara nyingi wateja, kwa mfano shule, wanaagizo idadi kubwa.
Mara nyingine paa nzima inaandaliwa kiwandani na baadaye mafundi wanaiweka juu ya nyumba.















