Kupokelewa katika Utawa

Tunapokea kijana yeyote wa kiume anayejisikia wito wa kujiunga nasi. Awe amehitimu kidato cha nne au cha sita na kufaulu kwa kiwango cha daraja I, II au III.
Aidha pia aliyehitimu kidato cha nne au cha sita pamoja na ufundi katika fani fulani.
Pia tunawakaribisha wote waliohitimu mafunzo ya elimu ya juu.

Mwombaji atume barua ya maombi kwa Mkurugenzi wa Miito, Abasia ya Mt.Benedikto Peramiho.
Ikisha kupokelewa, ataalikwa kwa wiki tatu na kukaa na jumuiya ili kujifunza maisha ya kitawa, huitwa kipindi cha kufahamiana.

Muda wa Malezi

Ukandidati na upostulanti ni mwaka mmoja na nusu. Unovisi mwaka mmoja. Halafu uprofesi wa muda (Nadhiri za muda).


Br.Albert akimpongeza mtawa mpya Br.Mauro kwa kufunga nadhiri