Girls' Secondary School

Hata siku hizi watoto wengi, hasa wasichana, hawaweza kusoma shule za sekondari.

Wakati masista Wabenediktini Wamisionari wa Tutzing walipoanzisha shule ya sekondari ya wasichana mnamo mwaka 1968, hali ya elimu ilikuwa mbaya zaidi. Wanaume wengi, hata baadhi ya mapadre, walifikiri elimu ya wasichana si kitu cha maana. Hata hivyo masista walizindua shule hii ya wasichana.

Shule ni shule ya bweni, wanafunzi wote wanaishi shuleni.

Masista watatu na mmonaki wa Abasia ya Peramiho wanafundisha dini, ujuzi wa biblia na hisabati.


Chakula cha kila siku