Kituo cha umeme Likingo
Kituo cha umeme Likingo kipo umbali wa km 25 kutoka Peramiho. Mito Luhira na Mkingazi imekutana pamoja na kusababisha maporomoko ya mita 45. Tunatumia maporomoko hayo ya asili kuzungusha magurudumu mawili yanayozalisha umeme kiasi cha kW 500 kwa jumla. Magurudumu hayo mawili na jenereta mbili huzalisha umeme wa kW 250 kila moja.
Umeme kutoka Likingo unasafirishwa mpaka Peramiho kwa njia ya waya wa ardhini unaochukua kiasi cha kV 11. Umeme huo ndio unaosaidia kuendesha hospitali, viwanda, mashule na nyumba za watawa.
Kituo cha umeme cha maji hakitoi gesi ya aina yoyote, hivyo hakisababishi kuharibika kwa hali ya hewa (climate change) kwa namna yoyote. Hapa Peramiho kuna njia nyingine ya kupata umeme, yaani kuendesha jenereta za diesel. Jenereta hizo zinaharibu hali ya hewa na pia kugharimu sana. Lakini siku nyingine kabla mvua hazijaanza kunyesha, tunapata umeme kwa njia ya jenereta za diesel. Kila siku yanahitajika mafuta ya gharama kama kiasi cha Shilingi 1,500,000.














