Jatropha - Kupata Umeme bila Kuharibu Hali ya Hewa

Tunaendesha kituo cha umeme wa maji. Hata hivyo tunahitaji pia umema wa diesel, kwa sababu kila mwaka mwishoni kwa kiangazi maji yanapungua sana. Kutumia jenereta ya diesel kunagharamu sana na pia jenereta inatoa gesi aina ya carbon dioxide, gesi inayoharibu hali ya hewa kwa kiasi kikubwa.

Hivyo tuliamua kubadilisha mafuta na kutumia "green energy". Mwezi wa 9 mwaka 2007, yaani miezi miwili kabla mvua hazijaanza kunyesha, tulipanda mimea ya jatropha. Mvua zilipoanza kunyesha, miche ilihamishwa kutoka kitaluni kwenda kupandwa kwenye shamba kubwa zaidi. Baada ya miaka mitatu mimea itazaa matunda yenye mafuta mazuri sana kwa kuendesha jenereta.

Mimea inapozaa matunda yao, inavuta carbon dioxide (CO2) kutoka hewani. Hivyo kwa jumla umeme wa jatropha hausababishi kutoa CO2 (zero emission) na kutosababisha kuharibu hali ya hewa.

Kuendelea


Wafanyakazi wa shamba la jatropha