Hospitali ya Misheni ya Mt. Josefu

Hospitali ya Peramiho inatibu wagonjwa waliolazwa wapatao 17,000 kwa mwaka. Karibu nusu ya hao wanasumbuliwa na malaria, kama akina mama 3,000 wanafika kujifungulia hapa hospitalini. Kama watu 120,000 wanafika kwa matibabu bila kulazwa.

Daktari Bruda Ansgar Stüfe O.S.B anafanya kazi kama mkurugenzi mkuu, Daktari Lemuel (Lemmy) Rugumyaheto ni makamu na Daktari Venance Mushi ni mganga mkuu. Baada ya Br. Ansgar kuteuliwa kuwa mhasibu mkuu wa shirika letu, kazi yake kubwa alikabidhiwa Daktari Lemmy.

Mnamo mwaka 1901 masista wamisionari wa kwanza walifika hapa Peramiho, kati ya hao mmoja alikuwa mwuguzi. Hivyo uuguzi ulianza hapa Peramiho miaka mitatu tu baada ya kufika kwa wamisionari wa kwanza. Mwaka 1923 vibanda kwa ajili ya kulaza wagonjwa vilijengwa. Ilipofikia mwaka 1949 daktari wa kwanza alifika hapa Peramiho Sr.Daktari Tetwigis Sailer O.S.B. Mwaka ule hospitali ilitambulishwa rasmi.

Kuendelea


Uuguzi wakati wa mwanzo wa hospitali