Hospitali ya Misheni ya Mt. Josefu (inaendelea)

Kuanzia mwaka 1980 hadi mwaka 1994 tuliweza kuongeza majengo ya hospitali kwa msaada wa shirika katoliki la kijerumani liitwalo MISEREOR.

Br.Dr. Ansgar Stuefe O.S.B. alifika mnamo mwaka 1987 na alifanya kazi kama mmonaki wa kwanza hospitalini. Tangu 1901 masista wamisionari wa Tutzing walitibu wagonjwa peke yao. Enzi ya mganga mkuu Br.Ansgar kilikuwa kipindi cha kuongeza watumishi wa hospitali (siku hizi kama 300) na pia idadi ya vitanda (kwa sasa 420).

Siku hizi hospitali inajali sana maarifa ya watumishi wake na umuhimu wa kutunza afya vijijini. Kazi ya udaktari katika mazingira ya umaskini daima ni ngumu. Kupata aina mbalimbali za dawa za kutosha na kutunza vyombo kweli ni changamoto. Idadi kubwa ya wagonjwa wanaotafuta msaada wetu, hasa kutoka Songea mjini, inaonyesha maana ya kazi yetu kwa ajili ya wanadamu wa nchi yetu.


Br.Dr.Ansgar akipima uzito wa mtoto mchanga