Picha inaonyesha mwanzo wa kuuguza wagonjwa hapa Peramiho, masista wa Ulaya na masista wa Afrika wabenediktini walikuwa wanatibu vidonda. Madaktari wa zamani waliwashauri Wazungu kuvaa kofia zinazoonekana kwa ajili ya kuwalinda dhidi ya jua kali la Afrika. Lakini siku hizi madaktari wanacheka kuhusu ule ushauri wa zamani, kwa sababu wanajua kwamba kofia yoyote yenye ncha pana inatosha kwa kulinda kichwa. Soma zaidi...